Sidebar Menu

News and Stories

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Praesent vulputate venenatis magna ut tempus.

25 October 2019 Dodoma. Kama njia ya kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la afya, Vision Sports wanawaletea Dodoma Marathon kwa msimu wa tatu mfululizo. Manispaa ya Dodoma itabadilika nakuwa mji kitovu cha furaha na utimamu wa mwili kwa familia nzima siku ya trh 9 Nov 2019 wakati ambapo mji utakapoandaa kupokea msimu wa tatu wa mbio hizi.

Tangazo limetolewa wakati wa mkutano wa pamoja na vyombo vya habari uliofanyika leo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Patrobas Katambi

Tunajisikia faraja kuwa waandaaji wa tukio ambalo si tu kwamba litaileta nchi pamoja lakini pia liaweza kuzitangaza tamaduni zetu pamoja na utalii alisema Mh. Patrobas Katambi. Kutokana na watu wengi wanaoingia katika jiji hili, tutashuhudia ukuaji katika shuguli za maendeleo ya kiuchumi. Alisema.

Mbio zitahusisha mbio ndefu za 42km, 21km,10km matembezi ya 5km na Watoto 2.5Km. huku zawadi zikitarajiwa kutolewa kwa washiriki watakaofanya vizuri katika 42km and 21km umbali shindaniwa. Wakimbiaji hodari wa mbio ndefu pamoja na wakimbiaji wapya kutoka pande zote za nchi hata nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizi zinazosubiliwa kwa hamu.Pesa taslimu zitatolewa kwa washindi wa mbio za 42.2Km na 21.1Km kwa wakwanza hadi wa kumi na yule wa kwanza wa 42.2Km kushindania Tsh 1,000,000/ na 21.1Km Tsh500,000/=. Washiriki wa Dodoma Marathon wote kupatiwa medali za ubora wakipekee nchini.

Tunajivunia kuandaa tukio hili linalowapa hamasa watu kuwa timamu kimwili na wenye afya ili watumie ujuzi wao kung’ara. Alisema Mratibu Bw. Ally Nchahaga. Tunafarijika kuona usajili umekuwa mkubwa mwaka hu una haswa wakazi wa Dodoma. Ni Imani yetu kadri miaka inavyokwenda ndivyo malengo yakufanya Jiji la Dodoma litambulike kwa mchezo huu kama majiji mengine duniani na kuzidi kuitambulisha Dodoma katika jumuiya ya kimaraifa

Mbio zote zitaanza na kuitimishwa katika uwanjan wa Jamhuri, Dodoma Marathon zitakuwa mbio kama zilivyo katika mashindano mengine. Ikiwa na mwonekano mzuri wa kijiografia.

Dodoma Marathon is supported by Dodoma Regional Commissioner’s Office (RAS), Jambo Drinking Water, Red Bull, NHIF, Azam Media, Dudumizi, Automart and NAM Enterprises.